FastSaying

Mungu anataka tujifunike kwa ngao yake. Yaani, tuwe na imani iliyokomaa katika Bwana na yeye atatufunika. Maana ya kauli hiyo ni kwamba kila kiungo cha miili yetu kuanzia unyayo hadi kichwa lazima kifunikwe kwa silaha ya Mungu, ambayo Mungu anaiita panoplia. Panoplia haimo katika kamusi ya Kiswahili au Kiingereza, lakini maana yake ni ‘ngao kamili ya Mungu’. Hii si tu silaha ya Mungu. Ni silaha kamili ya Mungu tunayotakiwa kujifunika kwayo.

Enock Maregesi

Enock Maregesi

faithgodimanimungungaongao-kamili-ya-mungupanopliashieldsilaha-ya-munguweapon-of-god

Related Quotes

Kuwa na huruma kwa malaika anayekulinda ni kujifunika kwa silaha kamili ya Mungu. Ukijifunika kwa panoplia utamrahisishia kazi malaika wako, aliyepewa jukumu na Mwenyezi Mungu kukulinda.
— Enock Maregesi
angelcompassionfull-armor-of-god
Kuvunja sheria ni sawa na kufanya kosa, na kwa hiyo kuwa mkosaji, mbele ya sheria na mbele ya mungu.
— Enock Maregesi
before-godbefore-the-lawgod
Matatizo ya watu yamekuwa makubwa kuliko Injili. Mungu hasisimuliwi na matatizo yako. Anasisimuliwa na imani yako.
— Enock Maregesi
faithgodgospel
Mungu anaishi ndani ya damu, maisha ya Mungu yalikuwa yanaishi ndani ya mwili wa Yesu Kristo, anaishi ndani ya miili yetu. Unapokula damu, unapokunywa damu, unakula, unakunywa sehemu ya Mungu aliyekuumba.
— Enock Maregesi
blooddamugod
Mungu anataka nini zaidi kutoka kwako? Anakutaka wewe.
— Enock Maregesi
godmunguwewe